Kwa mujibu wa kifungu namba 16 cha sheria ya mtoto, mtoto anahitaji uangalizi maalumu endapo akiwa na sifa zifuatazo,
• Mtoto yatima
• Mtoto aliye na wazazi au walezi wasiotoa malezi bora
• Mtoto aliye chini ya malezi ya wazazi au walezi ambao ni walevi au kwa sababu za kiuhalifu hawafai kuishi na mtoto huyo.
• Mtoto ambaye anatendewa ukatili na wazazi au walezi wake
• Mtoto ambaye anahusishwa na ukahaba au kuishi na walezi au wazazi wanaotuhumiwa kufanya ukahaba.